🤍 MAHUSIANO YANAHITAJI WATU WAWILI WANAOTAKA KUJENGA
Huwezi kujenga mahusiano peke yako.
Mtu mmoja akijitahidi kuwasiliana na mwingine anakataa kuzungumza, inakuwa vigumu. Mmoja akiheshimu na mwingine kudhalilisha, kuna tatizo. Mmoja akipanga maisha na mwingine hana nia ya kushirikiana, safari inakuwa nzito.
Mahusiano si mashindano ya nani yuko sahihi zaidi. Ni ushirikiano wa watu wawili wanaotaka kuona maisha yao yakiwa bora.
Kabla ya kumuuliza mwenza wako anafanya nini kwa ajili yako, jiulize pia: “Mimi ninafanya nini ili mahusiano haya yawe bora?”
Upendo wa kweli una uwajibikaji kutoka pande zote.
💫www.Letaplus.online⚡
