💔 USISHIKILIE MAHUSIANO YANAYOKUPOTEZEA WEWE
Kuna tofauti kati ya kupigania mahusiano na kujipoteza ndani ya mahusiano. Kupigania ni kutafuta suluhisho, kuzungumza na kuvumilia changamoto zinazoweza kutatuliwa. Kujipoteza ni kuendelea kuvumilia kila kitu mpaka unapoteza heshima yako, amani yako na utu wako.
Upendo haupaswi kukufanya uogope kila siku. Haupaswi kukufanya ujione huna thamani. Haupaswi kukulazimisha kubadilisha kila kitu kuhusu wewe ili tu mtu mwingine aridhike.
Mahusiano yenye afya yanawafanya watu wawili wakue pamoja, si mmoja kumdhibiti mwingine.
Kama kuna tatizo, zungumzeni. Kama kuna kosa, rekebisheni. Kama kuna tofauti, tafuteni njia ya kuelewana. Lakini usisahau kwamba kujipenda na kujiheshimu ni sehemu muhimu ya kumpenda mtu mwingine.
