🌐 Intaneti: Fursa kubwa lakini inahitaji busara
Intaneti imetoa nafasi kubwa sana kwa watu kujifunza, kufanya biashara na kupata taarifa.
Lakini si kila kitu unachokiona mtandaoni ni cha kweli.
Kuna taarifa za uongo, matangazo yanayopotosha, akaunti bandia, tovuti zisizoaminika na watu wanaoweza kutumia mbinu mbalimbali kukushawishi utoe taarifa zako.
Kwa hiyo, kabla ya kuamini taarifa fulani, chunguza chanzo chake.
Usikimbilie kushiriki taarifa kwa sababu tu imeonekana kwenye WhatsApp, Facebook, TikTok, Telegram au platform nyingine.
Jiulize:
Taarifa hii imetoka wapi?
Chanzo chake kinaaminika?
Kuna ushahidi?
Taarifa hii inapatikana pia kwenye chanzo rasmi?
Hii ni sehemu ya kuwa mtumiaji mwenye akili katika dunia ya teknolojia.
💫www.Letaplus.online⚡
